Visit our
Main Page at
www.sowitec.com

Kwa mstari mbele katika kutayarisha miradi ya stima kutokana nishati ya jua na upepo

Maono yetu ni kutengeneza miradi ya stima kutokana na nishati ya jua na upepo ambazo hatimaye zitawezesha Wakenya kupata kawi safi na kuwezesha Kenya kuendeleza sekta ya kawi pungufu na kaboni na kuimarisha usalama wa kawi.

Kampuni ya SOWITEC kilianzishwa mnamo 1993 Ujerumani na kimekuwa nchini Kenya tangu 2015. SOWITEC kinatayarisha miradi ya stima kutokana na nishati ya jua na upepo nchini mzima. Stima hii huunganishwa kwenye mtandao wa stima wa kitaifa. Tuko na mradi bomba ya takriban 600MW.

SOWITEC Kenya hufanya kazi pamoja na jamii mradini, washikadau na wawekahazina kuambatana na viwango vya juu vya kutayarisha miradi kuhakikisha si tu ufanisi wakifundi wa mradi bali pia kupatikana kwa thamani kwa jamii mradini.

Mfumo wetu wa uendelevu umeshilikilwa katika utoaji wa miradi ya stima ya nishati ya jua na upepo yaliyo safi na ya ushindani na pia yenye manufaa shirikana kwa jamii mradini. Desturi zetu za kibiashara zinashawishiwa na viwango vya kimataifa vya maadili, uwazi, usalama, kujitoelea kwetu kwa kulinda mazingira na jamii na uendelevu.

 

Timu

SOWITEC Kenya ni timu ya wajuzi kutoka sekta mbalimbali yakiwemo wahandisi, wanasheria na wajuzi katika maswala ya mazingira na uhusiano na jamii. Pamoja tunaendeleza maono ya SOWITEC ya kubadilisha sketa ya stima duniani kuwa na kawi safi na iliyo na bei nafuu kwa wote. Nchini Kenya tunatilia mkazo mawasiliano na jamii miradini na kujumulishwa kwa vikundi vilivyogandamizwa katika jamii. Kama timu tunajikakamua kujifunza na kujiboresha kila siku na kuboresha ubora wa miradi zetu.

 

Huduma zetu

SOWITEC Kenya huwasilisha thamani kupitia kuelewa kwa mazingira ya biashara ya kawi Kenya, mawasiliano bora na serikali na ofisi zake mbalimbali na ujuzi katika mawasiliano na jamii miradini. SOWITEC Kenya ina utaalamu na uzoefu katika utathmini wa miradi ya stima kutokana na nishati ya jua na upepo kwa eneo za kifundi, kisheria na kiuchumi. Kituo cha Ubora cha SOWITEC kinauwezo wakutoa huduma za aina zote katika harakati ya kutayarisha miradi ya stima kutokana na nishati ya jua na upepo. Haya yakiwemo:

  • Kubuni kwa miradi mpya
  • Usawashaji wa hatimiliki za shamba
  • Majadiliano ya kandarasi za kukodisha shamba
  • Upimaji raslimali ya Jua na Upepo
  • Utafiti wa athari kwa mazingira
  • Micrositing
  • Utafiti wa athari kwa jamii
  • Mawasiliano na Jamii mradini
  • Utafiti wa athari kwa mtandao wa stima
  • Utafiti wa kiramani, mandhari na jiografia la eneo la mradi
  • Uhandisi wa ujenzi na umeme
  • Kupata Liseni kwa mradi
  • Utafiti na kuhesabu kwa uchumi wa mradi
  • Uendelezaji wa biashara, ufadhili na unyinyaji wa kibiashara

Mazingira na jamii

Uendelevu umewekwa katika mazoea yetu ya biashara na ushirikiano na wamiliki wa ardhi na wadau. Hii inatuwezesha kujenga imani na kuendeleza maono pamoja nao katika kutayarisha ya miradi yetu.

SOWITEC inahusisha wamiliki wa ardhi, wadau na jumuiya mapema katika kutayarisha kwa miradi na kuwaona kama muhimu kwa mafanikio ya miradi yetu. Ubunifu wa mradi unatengenezwa kwa kushauriana na wamiliki wa ardhi na wadau wanaohusika.

SOWITEChufanya tathmini ya athari za mazingira na kijamii ili kutambua uwezekano wa mathara yoyote ya mradi kwenye mazingira na jamii. Wakati wa kubuni wa mradi, mipango ya kuboresha hali ya mazingira na kijamii inatambuliwa na kutekelezwa katika awamu ya utekelezaji wa miradi.

MAADILI NA UADILIFU

Tunaelewa kwamba kufanikiwa katika shughuli za biashara yetu, kunahitaji maadili na viwango vya juu vya uadilifu. Utekelezaji wa kazi kwa uadilifu ni kanuni muhimu katika mikakati ya kazi ya SOWITEC, na ndio muundo msingi wa maendeleo endelevu na ustawi wa SOWITEC na jamii zinazozingira miradi yetu.

Karibu kwenye kituo cha mawasiliano ya maadili ya SOWITEC:
Hiki ni kituo cha kuwasiliana na kuriporti matukio yanayodaiwa au kushukiwa kukiuka kanuni na sera za SOWITEC (yakiwemo Kanuni ya Maadili [SOWITEC Code of Conduct], Kanuni za Wahusika Wasio wa Moja kwa Moja [Compliance Rules for Third Parties], na sera za kampuni), na ikijumuisha pia sheria na kanuni zozote zinazohusika na biashara ya SOWITEC. Mawasiliano yanayoripotiwa hapa yatashugulikiwa kwa siri na uangalifu kwa wanaohusika. Wanaoripoti wanaweza kutujulisha kama hawangependa kujulikana.

Unaweza kuripoti tukio ukitumia njia hizi:
E-mail: ;

Wasiliana nasi

SOWITEC Kenya Limited
The Promenade, General Mathenge Drive
P.O. Box. 38265-00623
Nairobi
Kenya

 

+254 725022717
Please calculate 7 plus 1.